TCRA|Tanzania Communications Regulatory Authority
   
 

 

 

 

 

 

 

Consumer Affairs

Complaints

FAQ

Feedback

Know your Rights
  
Tariffs Info
 
Headlines
 
  • Uhusiano Baina ya Mionzi Itokayo Kwenye Vyombo vya Mawasiliano ya Simu na Utangazaji na Afya ya Binadamu
    Miaka ya hivi karibuni hapa nchini Tanzania na seheme nyingine duniani kiwango cha matumizi ya vyombo vya habari na mawasiliano, ikiwa ni pamoja na simu,minara ya mawasiliano, radar, redio, televisheni, kompyuta na kadhalika kimeongezeka sana. Matumizi yamefanya wananchi wengi kujiuliza uhusiano wa vyombo vya mawasiliano na afya zao.

    Kwa kuzingatia maoni mbali mbali yaliotolewa na wadau wa mawasiliano na wananchi kwa ujumla Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania inapenda kutoa ufafanuzi ufuatao:
    1. Mionzi inayotoka kwenye vyombo vya mawasiliano kama vilivyotajwa hapo juu yapo kwenye kiwango cha chini sana kuweza kumdhuru binadamu. Kiasi cha mionzi hiyo ni sawa na kile kilichothibitishwa na mashirika mbali mbali ya kimataifa kufuatia utafiti uliochukua takriban miaka 50. Mashirika yaliyohusika katika utafiti huo ni pamoja na:
      • Shirika la Umoja wa Mataifa la Mawasiliano ya Simu (International Telecommunications Union - ITU);

      • Shirika la Afya Ulimwenguni (World Health organization - WHO);

      • Tume ya Kimataifa ya Kinga Dhidi ya Mionzi (International Commission on Non-ionizing Radiation Protection - ICNIRP)

      • Chama cha Mawasiliano ya Simu za Mikononi (GSM Association);

      • Muungano wa Watengenezaji wa Simu za Mikononi (Mobile Manufacturers Forum - MMF).

    2. Ziko taarifa nyingi sana zitokanazo na utafiti wa kisayansi juu ya athari za
      masafa (the radiofrequency-RF) kwa afya ya binadamu. Kipimo cha jinsi mionzi inavyoingia kwenye mwili wa binadamu huitwa “Specific Absorption Rate (SAR)”. Taarifa hizo zinaonyesha kuwa nguvu ya mionzi ipo chini ya kiwango fulani (threshold) hayana athari kwa mwili wa binadamu. Nguvu za mionzi hupungua toka chanzo cha mionzi hiyo (inverse sqruare law). Kutokana na utafiti wa ICNIRP na ITU, SAR ni Watt 2 kwa uzito wa kilo moja (2 W/kg kwa kichwani na kiwiliwili) na Watt 4 kwa uzito wa kilo moja (4 W/kg kwa miguuni na mikononi) kwa umma na vipimo vikubwa zaidi ya haivyo kwa wafanya kazi wa mawasiliano wakiwa kwenye mitambo ya mawasiliano.

    3. Mawimbi ya umeme na sumaku (electromagnetic waves) yako ya aina nyingi, kwa mfano: mawimbi ya radio, mawimbi ya microwave, infrared, mwanga wa kawaida, ultraviolet, X-ray, gamma rays(mawimbi yatokanayo na nuklia), na kadhalika. Kama inavyoonyeshwa kwenye jedwali lililoambatanishwa na maelezo haya, nguvu ya mionzi ya redio iikiwa ni pamoja na simu ya mkononi ni kidogo ikilinganishwa na mwanga unaoonekana kwa macho. Vyanzo vya mionzi hii huweza kuwa ama vya asili au mitambo mbali mbali. Minara ya mawasiliano huwa na urefu wa mita 15 hadi 50 au kwenye majumba marefu, kwa hiyo nguvu inayomfikia binadamu ni ndogo.

    4. Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imekuwa ikifanya jitihada kushawishi watoa huduma za mawasiliano na utangazaji kushirikiana kutumia minara (infrastructure sharing). Hatua mojawapo iliyochukuliwa ni kutoa mfumo mpya wa leseni (Converged Licensing Framework) ambao una leseni nne: Leseni ya miundombinu (Netwwork Facility License), Leseni ya kutoa huduma (Network Service License), leseni ya matumizi (Application Service License) na leseni ya utangazaji (Content Service License). Vile vile Mamlaka imetoa kanunu za mawasiliano za 2005 ambazo zinawashawishi watoa huduma kujenga minara na kukodisha wa wengine badala ya kila mmoja kuwa na mnara wake mwenyewe.

    5. Kuna tafiti nyingi zimefanyika ambazo zimeonyesha kwamba kiwango cha
      mawimbi ya mawasiliano hakina madhara kwa afya ya binadamu. Mamlaka inashauri watumiaji wa huduma na wananchi wote kuendelea kuwa na imani na teknolojia mpya ikiwemo ya mawasiliano ya simu, utangazaji na utumiaji wa kompyuta ambazo hutumiwa ulimwenguni kote bila kuleta madhara yoyote. Maelezo haya yametokana na tafiti mbalimbali na maelezo mengine imebidi kutumia lugha ya kitaalamu. Iwapo yatahitajika maelezo zaidi au kama kuna malalamiko yoyote kuhusu mawasiliano, Mamlaka ipo tayari kutoa ufafanuzi na kuyafanyia kazi maswala yote.


    Imetolewa na:

    Mkurugenzi Mkuu

    Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania
     
  • Comment to Webmaster
    TCRA All Rights Reserved.  ©2006