Bi. Rehema Jessica Khalid
Mjumbe wa BodiRehema Jessica Khalid ni Wakili wa Mahakama Kuu ya Tanzania mwenye Shahada ya Uzamili ya Sheria, iliyojikita katika Sheria za Kampuni. Ana Shahada ya Kwanza ya Sheria ya Chuo Kikuu cha Bangalore, India. Kwa sasa ni Katibu na Mwanasheria Mkuu wa Mkulazi Holding Company Limited (MHCL).
Nafasi nyingine alizowahi kushika ni pamoja na Mshirika kwenye Kampuni ya Wanasheria ya Precise Law Attorneys kuanzia Agosti 2018 hadi Juni 2019, Mkuu wa Idara inayosimamia majukumu ya kampuni na masuala ya kisheria ya Zantel kati ya Juni 2014 na Julai 2018, Mwanasheria Mwandamizi wa Mkono and Company Advocates kati ya Januari 2007 na Juni 2014.
Rehema Jessica Khalid ni mjumbe wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Taasisi ya Wakurugenzi (IoDT) Tanzania na Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB).