TANGAZO LA KUFUTWA KWA LESENI ILIYOTOLEWA KWA KAMPUNI YA AUGERE TANZANIA LIMITED

(Limetolewa chini ya kifungu 22 cha Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta, cap 316).

KWA KUWA tarehe 1 Juni 2011 Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (ambayo kwenye tangazo hili itaitwa MAMLAKA) ilitoa leseni kwa kampuni ya AUGERE TANZANIA LIMITED (ambayo kwenye tangazo hili itaitwa MWENYE LESENI) kutoa huduma za kujenga miundombinu, kutoa huduma kupitia miundombinu hiyo,   kutoa huduma kupitia mtandao wa mawasiliano na kutumia masafa ya mawasiliano kitaifa;

NA KUWA MWENYE LESENI ameshindwa kujenga miundombinu na kuanza kutoa huduma kwa wateja; ambavyo ni ukiukwaji mkubwa wa masharti ya leseni alizopewa kama ilivyoainishwa kwenye kifungu 21(a) na (b) cha Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta Cap. 306;

NA KWA KUWA MWENYE LESENI ameshindwa kulipa ada za leseni hizo kama inavyotakiwa chini ya kifungu 15 (1) cha Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta, Cap. 306;

NA KWA KUWA kwa mujibu wa kifungu 6(3) cha Sheria ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, Cap. 172, MAMLAKA imewasiliana na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiiano kuhusu kufutwa kwa LESENI hizo.

KWA HIYO SASA, kwa uwezo iliyopewa Kisheria, MAMLAKA inafuta LESENI zote zilizotolewa kwa AUGERE TANZANIA LIMITED.

IMETOLEWA NA:

MKURUGENZI MKUU
MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA

MACHI,2016

Contact Details

20 Sam Nujoma Road
+255 22 2199760-8 More +

Staff Mail

isotext

Connect with us

Useful Links

  • used jeep for sale canada