JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA

TAASISI YENYE VIWANGO VYA ISO 9001: 2015

Makumbusho ya Mawasiliano TCRA, ilifunguliwa rasmi mwaka 2015 kwa lengo la kukusanya, kuweka kumbukumbu, kuhifadhi, kuonesha, kutafiti na kutoa elimu kuhusu historia na mabadiliko ya teknolojia za mawasiliano. Makumbusho inaonyesha historia na mabadiliko ya huduma za mawasiliano katika maeneo matano ambayo ni mawasiliano ya jadi, mawasiliano ya posta, mawasiliano ya simu, mawasiliano ya utangazaji na TEHAMA.

Makumbusho ya Mawasiliano TCRA ni kituo cha kujifunzia, kufanya utafiti na kukufanya uburudike kwa kukuonyesha vifaa mbalimbali vya kihistoria vya mawasiliano vilivyokusanywa vyenye thamani vikiakisi hatua mbalimbali za mabadiliko ya teknolojia nchini Tanzania. Vifaa vilivyokusanywa kwenye Makumbusho ya TCRA vina umuhimu mkubwa kwa wanafunzi na wanazuoni kuwawezesha kufanya utafiti kwenye sekta ya mawasiliano.  Pia, makumbusho ya mawasiliano inawapokea wananchi wote.

Muda wa Kufunguliwa

Jumatatu – Ijumaa, saa 3:30 Asubuhi hadi saa 9:30 Alasiri.

Kiingilio: Hakuna

ZINGATIA: Makumbusho ipo wazi siku za kazi tu, isipokuwa siku za sikukuu za kitaifa

Vifaa vinavyoonyeshwa

  • Maonyesho ya mawasiliano ya asili.
  • Maonyesho ya mawasiliano ya posta.
  • Maonyesho ya mawasiliano ya simu.
  • Maonyesho ya utangazaji.
  • Maonyesho ya vifaa vya TEHAMA

Picha na maelezo viwekwe hapa…

Ili kuchangia vifaa vya TEHAMA kwa makumbusho ya Mawasiliano, tafadhali wasiliana na Mamlaka kupitia:

Baruapepe: dg@tcra.go.tz

Simu ya bure kituo cha huduma kwa wateja: 0800008272

Je, una Maswali yoyote juu ya Sekta ya Mawasiliano?
Tuma Mrejesho na Malalamiko!

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imejidhatiti kutoa huduma bora kwa wateja na wadau wake wote.

Tuma Mrejesho na Malalamiko!