JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA

TAASISI YENYE VIWANGO VYA ISO 9001: 2015

Kitengo cha Huduma za Sheria za Taasisi

  1. Kutoa ushauri na msaada wa kisheria kimkakati;
  2. Kutumika kama Katibu kwenye vikao vya menejimenti na Bodi;
  3. Mtunzaji wa Nyaraka za Kisheria na Muhuri wa Mamlaka;
  4. Kuandaa Nyaraka za Kisheria za mamlaka;
  5. Kusimamia na kuratibu kesi za mamlaka na mashauri mengine ya kisheria ambayo Mamlaka inahusika;
  6. Kupitia upya na kuhakiki Sheria, Miongozo, Kanuni na mambo yanayohusiana nayo kulingana na  majukumu ya kisheria ya Mamlaka;
  7. Kushiriki katika majadiliano yote yanayohitaji utaalamu wa kisheria na kuiwakilisha Mamlaka katika Mashauri na Mashtaka ya Kimahakama;
  8. Kuiwakilisha Mamlaka kwenye masuala ya Usuluhishi na Upatanishi;
  9. Kuratibu shughuli za mashirika ya Kikanda na Kimataifa yanayohusika na maendeleo ya sekta za udhibiti kuhusiana na Masuala ya Sera na Sheria;
  10. Kuratibu mara kwa mara uhusiano na watoa huduma za kisheria wa nje

Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani

  1. Kuratibu,Kusimamia na kupitia Ukaguzi wa Fedha, Ukaguzi wa Utendaji, Ukaguzi wa Mifumo na Ukaguzi wa Kuthamini Fedha;
  2. Kuhudumu kama Sekretarieti katika Kamati ya Bodi ya Usimamiaji wa Ukaguzi na Vihatarishi;
  3. Kupitia na kuripoti kuhusu udhibiti stahiki wa mapato, utunzaji na matumizi yote ya rasilimali fedha za Mamlaka; 
  4. Kuandaa Mpango Mkakati na Mpango wa Ukaguzi wa Mwaka wa Mamlaka;
  5. Kufanya ukaguzi na udhibiti wa ndani na kuishauri menejimenti kuhusu utoshelevu wa mifumo ya ndani ya udhibiti;
  6. Kupitia na kuripoti kuhusu ufuataji wa taratibu za fedha na uendeshaji;
  7. Kupitia na kuripoti kuhusu kuaminika na ukamilifu wa data za fedha za kiuendeshaji;
  8. Kupitia na kuripoti kuhusu utoshelevu wa hatua zinazochukuliwa na menejimenti kutokana na Ripoti za Ukaguzi wa Ndani, na kuishauri menejimenti kuhusu utekelezaji au ushauri uliotolewa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu;
  9. Kufanya ukaguzi wa utendaji kuhusu tathimini ya miradi ya maendeleo;
  10. Kushirikiana na wakaguzi wa nje kuhusu ukaguzi wa kila mwaka na kuhakikisha kwamba  ripoti za Wakaguzi wa Nje hufuatwa na kutekelezwa na menejimenti; na
  11. Kufanya Ukaguzi wa Ufuatiliaji mara kwa mara.

Kitengo cha Manunuzi

  1. Kuandaa Mpango wa Ununuzi wa Mwaka wa Mamlaka na mkakati wake wa utekelezaji na kuufungamanisha na Bajeti na Mpango Kazi wa Mwaka wa Mamlaka;
  2. Kutoa Mwongozo wa Kiufundi kwa Mamlaka katika maeneo mbalimbali ya Ununuzi;
  3. Kuhudumu kama Sekretarieti ya Bodi ya Zabuni ya TCRA;
  4. Kuandaa Makabrasha ya Zabuni na kuratibu maandalizi ya mikataba kwa Zabuni mbalimbali zilizoshinda;
  5. Kuratibu utekelezaji wa kusimamia mikataba mbalimbali
  6. Kushirikiana na Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma na Vyombo vingine vya Serikali vinavyohusika na masuala ya Ununuzi;
  7. Kuandaa Ripoti za Mwezi na za Robo Mwaka kuhusu utekelezaji wa Mpango wa Ununuzi wa Mwaka;
  8. Kuimarisha na kuhifadhi kumbukumbu za michakato ya Ununuzi na kuondoa kwenye matumizi.

Kitengo cha Mawasiliano na Mahusiano kwa Umma

  1. Kuratibu na kuendesha Matukio ya uhusiano na Umma;
  2. Kuandaa  vitini vya matangazo na huduma rafiki kwa lengo la kutambulika na kujitangaza  na kuhakikisha usahihi na ufasaha;
  3. Kuandaa makala, ripoti na machapisho mengine;
  4. Kuandika na Kuhariri magazeti ya ndani pamoja na kudumisha na kuhuisha Tovuti ya TCRA na Akaunti  za Mitandao ya Kijamii;
  5. Kufuatilia mitazamo ya watu kuhusu Mamlaka kwa kuchambua kuripotiwa kwa TCRA katika vyombo vya habari, wadau na kuishauri menejimenti kwa mujibu wa mitazamo hiyo;
  6. Kusimamia Uhusiano na  Vyombo vya Habari;
  7. Kusimamia Bajeti ya Shirika ya uwajibikaji kwa jamii na kupitia maombi ya misaada;
  8. Kubaini Programu za Vyombo vya Habari, makala na Machapisho yanayofaa kutumika kusambaza taarifa za TCRA;
  9. Kusimamia uhusiano na wadau wengine na kuratibu shughuli za kiprotokali za TCRA; na
  10. Kusimamia shughuli za Maktaba ya Mamlaka.
  11. Kusimamia uendeshaji wa Makumbusho ya Mawasiliano

Kitengo cha kudhibiti Viashiria Hatarishi na Usimamizi wa Ubora wa Huduma

  1. Kutengeneza Mfumo wa Vihatarishi kwa ajili ya ukadiriaji na kutathimini ukabiliwaji na vihatarishi kwa Mamlaka kuhusiana na usalama, uwepo wa ulinzi, ulinzi wa data, ulinganifu wa kiudhibiti, Uendeshaji, uwajibikaji,  fedha na Vihatarishi vingine kwa kadri vitakavyokuwa vinabainishwa;
  2. Kufanya Ukadiriaji wa Vihatarishi kwa Ujumla na kuishauri menejimenti kama itakavyotakiwa;
  3. Kuandaa  Mwongozo wa Vihatarishi utakaotumika katika utambuaji na upunguzaji wa vihatarishi;
  4. Kufanya uchambuzi wa vihatarishi kwa ajili ya  njia mpya za kusimamia miradi, bidhaa na huduma, michakato na mifumo;
  5. Kuandaa ripoti kuhusu hali ya upunguzaji wa vihatarishi katika maeneo ya uwezekano wa vihatarishi yaliyokwishabainishwa awali;
  6. Kufanya upimaji wa hatua zilizochukuliwa na Kurugenzi na Vitengo mbalimbali ili kupunguza vihatarishi na kushauri ipasavyo;
  7. Kushauri kuhusu uthabiti wa hatua/taratibu za  upunguzaji vihatarishi zilizochukuliwa na Mamlaka;
  8. Kufanya upitiaji wa mara kwa mara wa masuala ya ulinganifu;
  9. Kufuatilia na kutekeleza mikakati mintarafu ya vihatarishi; 
  10. Pambanisha, jumuisha, fasiri na changanua ripoti za vihatarishi kutoka katika Mamlaka yote na kuunganisha ripoti zinazotakiwa; na
  11. Kuhakikisha kwamba usimamiaji wa vihatarishi umefungamanishwa katika Mamlaka yote.
  12. Kusimamia  Utengenezaji na utekelezaji wa Mfumo wa Usimamiaji Ubora, Sera ya Ubora na Malengo;
  13. Kuratibu utengenezaji wa QMS na Taratibu za Uendeshaji kwa utekelezaji mzuri wa Mfumo wa Usimamiaji Ubora;
  14. Kufuatilia utendaji wa Michakato ya ubora, Taratibu za Uendeshaji, Viwango na vipimo;
  15. Kutathmini mahitaji ya wateja na kuhakikisha kwamba yametimizwa na kuweka vipimo vya ndani vya huduma kwa wateja;
  16. Kuandaa na kuhuisha makabrasha ya ubora kwa mchakato unazingatia viwango vinavyotambulika kama vile Usimamiaji wa Ubora wa ISO 9000,unaochapishwa na Asasi ya Viwango ya Kimataifa;
  17. Kusimamia utekelezaji na ufuataji wa viawango na Mifumo ya Usimamiaji wa Ubora;
  18. Kusimamia, kufuatilia, na kupitia Taratibu za Uendeshaji na Michakato ya Mifumo ya Usimamiaji Ubora inayoathiri ubora wa huduma za Mamlaka;
  19. Kupanga, kutengeneza na kutekeleza Mifumo ya Usimamiaji Ubora na kinachofanyika katika chombo chote kwa kuzingatia sheria na viwango vilivyopo;
  20. Kufanya upitiaji wa mara kwa mara ili kujiridhisha na ufuataji wa Sera ya Viwango, Malengo, Michakato, Taratibu za Uendeshaji na Viwango kwa mujibu wa matakwa ya ISO;
  21. Kufanya Ukaguzi wa Ndani wa Mifumo ya Usimamiaji Ubora na kuandaa ripoti kwa ajili ya Vikao vya upitiaji vya  Menejimenti;
  22. Kushirikiana na Kurugenzi inayohusika na mafunzo na uendeshaji mafunzo yanayohusu viwango vya ubora;
  23. Kuratibu na kusaidia ukaguzi wa sehemu ya kazi unaofanywa na wakaguzi wa nje wa ISO;
  24. Kutathimini matokeo ya ukaguzi na kutekeleza ipasavyo marekebisho;
  25. Kufuatilia shughuli za usimamizi wa vihatarishi zilizomo katika Michakato ya Mifumo ya Usimamizi wa Ubora, na
  26. Kuendesha programu za uelewa kwa pande zenye nia ya kujua Mifumo ya Kusimamia Ubora ili kuimarisha masuala ya Mifumo ya Uendeshaji Ubora.
Je, una Maswali yoyote juu ya Sekta ya Mawasiliano?
Tuma Mrejesho na Malalamiko!

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imejidhatiti kutoa huduma bora kwa wateja na wadau wake wote.

Tuma Mrejesho na Malalamiko!