- Kusimamia maendeleo, utekelezaji na mapitio ya Kanuni, Sheria, na Miongozo ya utoaji leseni na usimamizi wa huduma za mawasiliano;
- Kusimamia utoaji leseni, matekelezo na Michakato ya Masuala ya Wateja;
- Kutoa ushauri kuhusiana na masuala ya Leseni na Utekelezaji wa sheria;
- Kuandaa ratiba ya kazi kwa ajili ya matekelezo ya masharti ya leseni na kusimamia utekelezaji;
- Kuandaa na kusimamia programu za masuala ya elimu kwa umma na wateja;
- Kusimamia maandalizi na utekelezaji wa mbinu za kushughulikia malalamiko;
- Kutoa Huduma za Sekretarieti kwenye Bodi, Kamati za Maudhui na Malalamiko za TCRA;
- Kuunganisha na Baraza la Ushauri wa Wateja la TCRA kuhusiana na masuala ya Wateja;
- Kuratibu shughuli za mashirika ya Kikanda na Kimataifa yanayojihusisha na masuala ya ACRAN.