JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA

TAASISI YENYE VIWANGO VYA ISO 9001: 2015

Sheria Na. 12 ya mwaka 2003 iliyoianzisha TCRA inaipa Mamlaka wajibu katika majukumu yafuatayo:

1. Kukuza ushindani bora na uchumi wenye tija;

2. Kulinda maslahi ya watumiaji;

3. Kulinda mitaji ya Watoa Huduma wenye ufanisi;

4. Kukuza upatikanaji wa huduma zinazodhibitiwa kwa watumiaji wote wakiwamo wenye kipato kidogo, walioko vijijini na watumiaji walio na walioko katika mazingira magumu;

5. Kuimarisha Elimu kwa Umma, uelewa na ufahamu  wa huduma zinazosimamiwa na TCRA, ikiwa ni pamoja na:

       (i) Haki na wajibu wa watumiaji na watoa huduma zinazosimamiwa;

       (ii) Namna ya kuwasilisha  malalamiko na migogoro na utaratibu wa utatuzi wake; na

       (iii) Kazi na majukumu ya Mamlaka kwa kuzingatia umuhimu wa kulinda na kutunza mazingira.

Je, una Maswali yoyote juu ya Sekta ya Mawasiliano?
Tuma Mrejesho na Malalamiko!

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imejidhatiti kutoa huduma bora kwa wateja na wadau wake wote.

Tuma Mrejesho na Malalamiko!