TCRA Kushiriki Kikao Kazi Cha 18 Cha Maafisa Habari na Mawasiliano wa Serikali Dar es Salaam,2023

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Bi. Lucy Mbogoro atatoa wasilisho kuhusu mfumo wa Leseni za Mawasiliano na namna ya kuomba leseni kupitia 'Tanzanite Portal.' Wasilisho litatolewa siku ya Jumanne, tarehe 28 Machi 2023 katika Kikao cha 18 cha Maafisa Habari na Mawasiliano wa Serikali (TAGCO) katika Ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Julius Nyerere, Dar es salaam.
Maafisa habari wote wa Serikali ambao wangependa kuanzisha Kituo cha Utangazaji wa Redio au Televisheni-mtandao (Online TV) wanahimizwa kushiriki ili kupata elimu ya utaratibu wa kuomba Leseni za Maudhui ya Utangazaji kupitia mfumo wa Tanzanite.