JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA

TAASISI YENYE VIWANGO VYA ISO 9001: 2015

Tunu Kuu

1. Weledi

Tunatekeleza majukumu yetu kwa kutoa huduma bora tukizingatia maadili na heshima  kwa wateja wetu;

2. Uwezeshaji

Tunawajengea uwezo wafanyakazi wetu ili kuwawezesha kukabiliana na  changamoto ikiwamo  kuwapa fursa za kufanya uamuzi wakati wanapotekeleza majukumu na kutimiza wajibu wao;

3. Ubunifu

Tunazingatia ubunifu katika kushughulikia masuala ya kiudhibiti sanjari na mabadiliko ya teknolojia duniani;

4. Uadilifu

Tunatekeleza kazi zetu kwa kuzingatia maadili, uthabiti na uaminifu wa hali ya juu; 

5. Utendaji wa Pamoja

Tunaamini katika utendaji kazi wa pamoja  ili kutatua matatizo na kutambua kwamba mawasiliano imara ni muhimu katika kujenga mazingira ya ushirikiano;

6. Uwajibikaji

Tunawajibika kikamilifu na kuchukua dhamana  tunapotoa huduma; na

7. Usawa

Tunaamini katika kutoa fursa na haki sawa kwa wadau wetu wa ndani na nje.

 

Malengo

Mamlaka imeandaa Malengo mbalimbali ili kufikia maono yake katika kukabiliana na mambo muhimu kama yalivyobainishwa katika uchambuzi wa hali halisi ya kisekta. Malengo hayo ni:-

  1. Kukuza miundombinu na huduma za mawasiliano ya kielektroni na posta yenye usalama, ufanisi na imara;
  2. Kuimarisha upatikanaji wa huduma za mawasiliano ya kielektroni na posta zenye ubora na unafuu;
  3. Kuimarisha ubunifu wa huduma zinazodhibitiwa, uandaaji wa maudhui ya ndani na ujanibishaji;
  4. Kuimarisha ufanisi wa huduma zinazodhibitiwa na kuwalinda wadau; na
  5. Kuimarisha uwezo wa taasisi.
Je, una Maswali yoyote juu ya Sekta ya Mawasiliano?
Tuma Mrejesho na Malalamiko!

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imejidhatiti kutoa huduma bora kwa wateja na wadau wake wote.

Tuma Mrejesho na Malalamiko!