Sheria Namba 12 ya mwaka 2003 iliyoianzisha TCRA inaipa Mamlaka wajibu katika majukumu yafuatayo:-
a) Kukuza ushindani bora na uchumi wenye tija;
b) Kulinda maslahi ya watumiaji;
c) Kulinda mitaji ya Watoa Huduma wenye ufanisi;
d) Kukuza upatikanaji wa huduma zinazodhibitiwa kwa watumiaji wote wakiwamo wenye kipato kidogo, walioko vijijini na watumiaji walio na walioko katika mazingira magumu;
e) Kuimarisha Elimu kwa Umma, uelewa na ufahamu wa huduma zinazosimamiwa na TCRA, ikiwa ni pamoja na:
i. Haki na wajibu wa watumiaji na watoa huduma zinazosimamiwa;
ii. Namna ya kuwasilisha malalamiko na migogoro na utaratibu wa utatuzi wake; na
iii. Kazi na majukumu ya Mamlaka kwa kuzingatia umuhimu wa kulinda na kutunza mazingira.