Idara ya Masuala ya Kisekta
- Kuchambua na kubainisha Ushuru wa forodha, Viwango, Kamisheni na tozo nyingine za huduma za mawasiliano;
- Kuratibu na kusimamia Mfumo wa mawasiliano ya simu (TTMS);
- Kufuatilia Sekta ya Mawasiliano na maendeleo ya udhibiti yanayoweza kuathiri majukumu ya Mamlaka;
- Kubainisha masoko ya mawasiliano na kupima ushindani kwenye masoko hayo;
- Kufanya uchunguzi na uchambuzi wa mara kwa mara wa mienendo ya uchumi mkubwa na maendeleo ya Sekta ya Mawasiliano;
- Kushughulikia uendeshaji wa jukwaa la ufuatiliaji wa biashara ya fedha kwa njia ya simu za mkononi;
- Kusimamia Rajisi Kuu ya Namba Tambulishi (CEIR) na kanzidata ya usajili wa laini za simu (SIM);
- Kufanya uchambuzi na ufafanuzi wa mara kwa mara wa takwimu kuhusu mienendo ya viashirio vya mawasiliano.