Mwanzo
Kuhusu
Huduma
Viunganishi
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA

TAASISI YENYE VIWANGO VYA ISO 9001: 2015

Ijue TCRA

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ni taasisi ya kiserikali yenye majukumu ya kusimamia sekta za Mawasiliano na Utangazaji Tanzania. Ilianzishwa kwa Sheria ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania Na. 12 ya mwaka 2003 kusimamia huduma za kielektroniki na posta na masafa ya mawasiliano katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mamlaka ilianza kazi tarehe 1 Novemba 2003 na inafanya shughuli za zilizokuwa Tume ya Mawasiliano Tanzania (TCC) na Tume ya Utangazaji Tanzania (TBC).

DIRA YETU

Kuwa Mdhibiti wa Mawasiliano ya Posta na Kielektroniki mwenye hadhi ya kimataifa

DHAMIRA YETU

Kusimamia huduma za Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta kwa ufanisi; kuboresha utendaji wa watoa huduma na kulinda maslahi ya watumiaji wa huduma za mawasiliano kwa lengo la kutoa mchango wetu kwa maendeleo ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

LENGO KUU

Kuboresha maisha ya Watanzania kupitia udhibiti wenye ufanisi, unaochochea na kukuza ubunifu na ambao unahakikisha kupatikana kwa huduma bora na imara za mawasiliano kwa wote na ambazo zinatolewa kwa gharama nafuu.

MALENGO MAKUU YA KIMKAKATI

  1. Kuzifanya shughuli za TCRA kuwa za kisasa kwa kutumia teknolojia sahihi; kuimarisha tafiti zenye ubora katika huduma zinazodhibitiwa, uwezo na umahiri wa watumishi.
  2. Kukuza ufanisi; kuaminika na kuhakikisha usalama wa miundombinu ya mawasiliano na matumizi yake.
  3. Kukuza ufanisi na unafuu wa huduma za Mawasiliano na kuongeza upatikanaji wa huduma za Posta na TEHAMA katika maeneo yasiyohudumiwa ipasavyo na yale yasiyo na huduma kabisa.
  4. Kulinda maslahi ya wadau na kukuza uelewa wa haki na wajibu wao.
  5. Kufuatilia utendaji wa huduma zinazosimamiwa na kuhakikisha utekelezaji wa Sheria na Kanuni kwa viwango vinavyostahili.
  6. Kuratibu utekelezaji wa ahadi za kisekta kitaifa, kikanda na kimataifa.

SERA YETU YA UBORA

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania imejikita katika kuhakikisha inafikia malengo yake ya kimkakati na kuhakikisha kwamba wateja wake wanaridhika na huduma zake zitakazotolewa kwa Mfumo wa Usimamizi wa Ubora.

MALENGO YA UBORA

  1. Kuboresha utaratibu na hatua za usimamizi wa sekta ya mawasiliano.
  2. Kufikia kiwango cha juu ya kuridhisha wateja kama ilivyoainishwa kwenye Mkataba wa Huduma kwa Mteja wa TCRA.
  3. Kuendelea kuzingatia matakwa ya kisheria na kiusimamizi.
© 2022 TCRA, Haki zote zimehifadhiwa.