Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA)(TCRA) ni mwanachama wa mashirika ya kikanda na kimataifa. Katika miaka iliyopita, TCRA imehudhuria mikutano na makongamano mbalimbali yaliyoandaliwa na baadhi ya mashirika haya yanayojihusisha na sekta ya mawasiliano. Baadhi ya mikutano hiyo ni pamoja na;
1. Mkutano Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Duniani (ITU-PP22)
Tanzania ni mwanachama wa Shirika la Mawasiliano Duniani (ITU), ambalo ni shirika maalumu linaloshughulika na Teknolojia za Habari na Mawasiliano (TEHAMA). Tanzania imekuwa mwanachama tangu mwaka 1962 na imechangia kwa kiasi kikubwa katika kazi na shughuli za umoja huo. Katika shughuli za ITU, Tanzania inawakilishwa na TCRA.
TCRA ilishiriki Mkutano Mkuu wa ITU mwaka 2022 (ITU-PP22) uliofanyika kuanzia tarehe 26 Septemba 2022 hadi tarehe 14 Oktoba 2022 jijini Bucharest nchini Romania. ITU PP ni chombo cha juu cha maamuzi cha ITU.
ITU PP-22 uliipa Tanzania na nchi nyingine 193 ambazo ni wanachama mtazamo wa kimkakati wa kusimamia sekta ya mawasiliano. Mkutano huo muhimu uliweka mipango, na tandaooo wake kwa miaka minne ijayo, kwenye maeneo yanayohusiana na tandaoo ya Mawasiliano ya simu /TEHAMA.
Katika tandao huo, Tanzania ilijadili masuala matatu muhimu, ambayo ni: kuwekeza nguvu zaidi katika rasilimali-watu na tandao; ushirikiano wa kimataifa katika kukabiliana na uhalifu mtandaoni; ulinganisho wa sera na mifumo ya kiudhibiti; uwiano wa sera na mfumo wa kisheria na tandaoo ya mkongo ili kufikia malengo ya muunganisho wa huduma za mawasiliano kikanda na ufikiwaji wa huduma kwa wote kwa nchi wanachama.
Pamoja na matukio mengine, Tanzania ilichaguliwa kuwa Mjumbe wa Baraza Kuu la ITU kwa kipindi ha miaka minne (2023 – 2026), kwa kupata kura 141 kati ya kura halali 180 zilizopigwa. Tanzania iliungana na nchi nyingine 47 zilizochaguliwa kwenye Baraza kwenye hilo.
2. Kamati ya Usimamizi wa Uchumi (Mkutano na Mafunzo)
Umoja wa Mamlaka za Usimamizi wa Mawasiliano kwa nchi za Kusini mwa Afrika (CRASA) uliandaa tandao wa pili wa Kamati ya Usimamizi wa Uchumi (ERC) uliofanyika kuanzia tarehe 21 hadi 26 Novemba 2022, Zanzibar chini ya uratibu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA) ambayo ni mwanachama wa shirika hilo.
Umoja wa Mamlaka za Usimamizi wa Mawasiliano kwa nchi za Kusini mwa Afrika (CRASA) unawakutanisha Wadhibiti wa sekta ya mawasiliano Kumi na tatu katika eneo la tanda mwa Jangwa la Sahara ambapo Tanzania inawakilishwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano ya Tanzania (TCRA).
Ajenda kuu ya Mkutano huo ilikuwa kuhakikisha wananchi katika nchi wanachama wanawezeshwa kumudu gharama za huduma za mawasiliano wanapovuka mipaka miongoni mwa nchi wanachama. Tanzania iliridhia kuchambua pendekezo la umoja huo la kupunguza gharama za mawasiliano katika ukanda wa SADC.
Mkutano ulitanguliwa na semina elekezi iliyolenga kuwajengea uelewa wajumbe kuhusu viashiria vya brodibendi, bei za huduma za mawasiliano, mtandao wa miundombinu ya mawasiliano, ukusanyaji, uchambuzi na uwasilishaji wa taarifa za gharama za mawasiliano.
- Pictures of the event
3. Siku ya Umoja wa Posta ya Afrika (PAPU) Mwaka 2023
Maadhimisho ya miaka 43 ya Umoja wa Posta ya Afrika (PAPU DAY) yalifanyika tarehe 13 Januari 2023 katika Mkoa wa Dodoma. Kauli mbiu ya maadhimisho hayo ilikuwa; “Posta: Mwezeshaji Mahiri wa Biashara Mtandao inayovuka Mipaka Barani Afrika.”
Kaulimbiu hiyo ililenga kutoa msisitizo kuhusu jukumu sahihi la sekta ya posta katika kukuza tandao o ya kiuchumi na jamii. Pia, tandao wa kuhakikisha kwamba, Tanzania inakwenda sanjari na dunia katika mageuzi ya kidijiti.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dkt. Jabiri Bakari, alihimiza sekta ya posta kuweka mazingira mazuri yanayowezesha ukuzaji biashara baina ya mipaka ambayo katika miaka ya karibuni imeongezeka kwa kasi katika nchi za Afrika. Pia, alielezea nia ya TCRA ya kushirikiana na wadau wote katika kuboresha mazingira hayo, ili kunufaika na fursa za biashara ya kidijiti.
4. Mkutano wa Mwaka wa TEHAMA,2022
Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA) ilishiriki Mkutano wa Mwaka wa TEHAMA, ambao ni miongoni mwa mikutano mikubwa ya wadau wa TEHAMA nchini.
TCRA ilishiriki mkutano huo kuanzia tarehe 26 hadi 28 Oktoba 2022 Zanzibar, ambao uliongozwa na kauli mbiu: Kuchangamkia Mabadiliko ya Kidijiti katika Uchumi wa Buluu kwa Maendeleo ya Kiuchumi na jamii.
Mkutano huo hutoa fursa ya kipekee ya kuwajengea uwezo wadau, majadiliano ya sera, kujenga mtandao wa wawekezaji wa biashara, mjadala wa kitaalamu, kubadilishana uzoefu kuhusu masuala ya TEHAMA, fursa za biashara, mahitaji ya maarifa na ujuzi ili kukabiliana na mabadiliko ya haraka YA katika ikolojia ya Kidijiti.
Katika mkutano huo, TCRA iliwasilisha dhamira yake ya kukuza matumizi ya TEHAMA na kuendeleza huduma mpya za mawasiliano zinazolenga kuboresha maisha ya watu.
TCRA ilitumia tukio hilo kuwasilisha jinsi inavyosaidia wabunifu wenye suluhisho mpya za TEHAMA ambazo zitawanufaisha moja kwa moja jamii. Hivi sasa, Serikali kupitia TCRA kwa kushirikiana na Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) inatoa rasilimali za mawasiliano bure kwa wabunifu chipukizi na vituo atamizi kwa kipindi cha miezi mitatu na muda wa majaribio unaweza kuongezwa ikiwa mradi unaohusika
5. Siku ya Mtandao Salama, 2023
Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA) iliratibu maadhimisho ya Siku ya Mtandao Salama ambayo yalifanyika tarehe 7 Februari 2023 katika Mkoa wa Dodoma. Mamlaka ilitumia siku hiyo kuwaelimisha vijana kuhusu Usalama wa mawasiliano ya Kielektroni na kuwahamasisha kuwa na ujuzi wa mtandao. Tukio hili linalenga kutambua, kuelimisha, na kujenga kizazi kijacho cha wataalamu wa usalama wa mtandao.
Kabla ya siku ya tukio, TCRA ilifanya juhudi za kutambua, kuhamasisha, na kusaidia ujuzi na utamaduni wa usalama wa mtandao kwa makundi mbalimbali yanayolengwa kama vijana kutoka shule za sekondari hadi taasisi za elimu ya juu kupitia programu mbalimbali za kujenga uelewa na mashindano ya usalama wa mtandao ambapo washiriki bora (Mabingwa wa Usalama Mtandaoni) walitambuliwa na kupewa zawadi.