JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA

TAASISI YENYE VIWANGO VYA ISO 9001: 2015

Sheria ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania ya mwaka 2003 (TCRA Act 2003) ndio iliyoanzisha kanuni za Sekta ya Posta ambapo TCRA imepewa jukumu la kusimamia utoaji wa huduma za Posta ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Sheria ya TCRA inazuia ufanyaji wa shughuli za Posta bila ya leseni halali inayotolewa na TCRA, TCRA pia inahakikisha uwapo wa huduma za posta zenye kuaminika, usalama, ufanisi na bei nafuu ndani ya Jamhuri ya Tanzania.

Kwa muktadha huu,TCRA imeandaa mazingira ya kudhibiti  utoaji wa huduma za Posta kwa kuandaa kanuni na nyenzo ambazo zitawezesha kufungua soko na kusaidia ubunifu katika utoaji wa huduma, hizi nyenzo za kudhibiti ni pamoja na Mfumo wa Leseni za Sekta ya Posta ambayo inatoa mwongozo wa utoaji leseni za posta nchini.

Utoaji wa Leseni za Posta

Mfumo wa Utoaji wa Leseni za huduma za Posta na zile za kusafirisha nyaraka, vifurushi na vipeto ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zimegawanyika katika makundi sita ambayo ni:

  1. Leseni Mtoa huduma za msingi za Posta: Leseni hii inatolewa kwa Shirika La Posta Tanzania (TPC) kwa kipindi cha miaka ishirini na Tano (25) ambayo inahuhishwa baada ya muda kuisha.
  2. Leseni ya Kimataifa ya Mtoa Huduma Binafsi ya Posta: Leseni hii inatolewa kwa watoa huduma binafsi ambao wanapokea, wanakusanya na kusambaza bidhaa za Posta (Nyaraka, vifurushi na vipeto) kutoka /kwenda nje ya nchi. Muda wa leseni hii ni miaka mitano (5) na inaweza kuhuishwa baada ya muda kuisha.
  3. Leseni ya Afrika Mashariki ya Mtoa Huduma Binafsi ya Posta: Leseni hii inatolewa kwa watoa huduma binafsi ambao wanapokea, wanakusanya na kusambaza bidhaa za Posta (Nyaraka, vifurushi na vipeto) kutoka /kwenda jumuiya ya Afrika Mashariki. Muda wa leseni hii ni miaka mitatu (3) na inaweza kuhuishwa baada ya muda kuisha.
  4. Leseni ya Ndani ya nchi ya Mtoa Huduma Binafsi ya Posta: Leseni hii inatolewa kwa watoa huduma binafsi ambao wanapokea, wanakusanya na kusambaza bidhaa za Posta (Nyaraka, vifurushi na vipeto) ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Muda wa leseni hii ni miaka mitatu (3) na inaweza kuhuishwa baada ya muda kuisha.
  5. Leseni ya Ndani ya mkoa mmoja nchini ya Mtoa huduma binafsi ya Posta:  Leseni hii inatolewa kwa watoa huduma binafsi ambao wanapokea, wanakusanya na kusambaza bidhaa za Posta (Nyaraka, vifurushi na vipeto) ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Muda wa leseni hii ni miaka mitatu (3) na inaweza kuhuishwa baada ya muda kuisha.
  6. Leseni ya kati ya vituo/mikoa miwili kwa msafirishaji nchini ya Mtoa huduma binafsi ya Posta: Leseni hii inatolewa kwa watoa huduma binafsi wa usafirishaji ambao wanapokea, wanakusanya na kusambaza bidhaa za Posta (Nyaraka, vifurushi na vipeto) kati ya vituo/ mikoa miwili ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Muda wa leseni hii ni miaka mitatu (3) na inaweza kuhuishwa baada ya muda kuisha.

Jedwali:: Ada za leseni za watoa huduma za Posta

Na.

 Kundi la Leseni

 Ada ya Maombi (Shs.)

Ada ya Mwaka wa kwanza (Shs.)

 Ada ya Maombi ya Kuhuisha (Shs.)

 Ada ya Mwaka (Shs.)

1

Mtoa Huduma za Posta za Msingi

           2,300,000

20,000,000

2,300,000

20,000,000

2

 Mtoa Huduma za Kimataifa

170,000

18,000,000

170,000

18,000,000

3

Mtoa Huduma ndani ya Afrika Mashariki

              100,000

   6,000,000

     100,000

   6,000,000

4

 Mtoa Huduma za Binafsi wa Ndani ya Nchi

                 60,000

    3,000,000

      60,000

   3,000,000

5

Mtoa Huduma binafsi ndani ya Mkoa mmoja

                 60,000

       1,400,000

       60,000

   1,400,000

6

Mtoa Huduma Binafsi wa Posta kati ya Mkoa miwili

                 60,000

       400,000

      60,000

       400,000

Unaweza kupakua kanuni za Mawasiliano ya Kielektroni na  Posta kwa upande wa leseni kwa kubofya https://www.tcra.go.tz/documents/regulations

Kwa ajili ya kuomba leseni bofya https://tanzanite.tcra.go.tz/login.htm

Kwa kutoa maoni/malalamiko https://www.tcra.go.tz/pages/complaints

Je, una Maswali yoyote juu ya Sekta ya Mawasiliano?
Tuma Mrejesho na Malalamiko!

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imejidhatiti kutoa huduma bora kwa wateja na wadau wake wote.

Tuma Mrejesho na Malalamiko!