JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA

TAASISI YENYE VIWANGO VYA ISO 9001: 2015

Ushirikiano Wa TCRA Na COSTECH, Kukuza Uchumi Wa Kidijitali

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), na Tume ya Sayansi na Teknolojia Tanzania (COSTECH) zimekubaliana kubadilishana rasilimali adimu za mawasiliano zikiwemo masafa na namba, zitakazoiwezesha COSTECH kuwahudumia wavumbuzi wa TEHAMA hasa Vijana kupitia vituo atamizi vya Teknolojia za Habari na Mawasiliano. 

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt. Jabiri Bakari (kulia) akibadilishana hati za makubaliano na Tume ya Sayansi na Teknolojia Tanzania (COSTECH), Dkt. Amos Muhunda Nungu, zitakazoshuhudia TCRA ikiipatia Tume rasilimali muhimu za Masafa ya Mawasiliano na namba fupi kwa wabunifu walioidhinishwa na Tume, ukiwa ni mkakati wa kukuza Uchumi wa Kidijitali Tanzania. Hafla hiyo ilifanyika katika Ukumbi wa Mawasiliano Towers jijini Dar es Salaam Hivi karibuni.

Je, una Maswali yoyote juu ya Sekta ya Mawasiliano?
Tuma Mrejesho na Malalamiko!

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imejidhatiti kutoa huduma bora kwa wateja na wadau wake wote.

Tuma Mrejesho na Malalamiko!