Makumbusho ya Mawasiliano
Makumbusho ya mawasiliano TCRA
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania imeanzisha makumbusho ya mawasiliano iliyoko makao makuu ya TCRA mjini Dar es Salaam. Makumbusho hayo, yaliyozinduliwa rasmi mwaka 2015 yana lengo la kutunza, kuhifadhi, kutafiti, kuonesha na kutoa elimu ya historia na ukuaji wa mawasiliano kiteknolojia. Makumbusho hayo yanaonesha mabadiliko katika mawasiliano ya posta, simu, utangazaji na njia za kale za mawasiliano.
Shughuli za makumbusho ya mawasiliano
- Kukusanya, kutunza na kuhifadhi taarifa za kihistoria na kiteknolojia kuhusu mabadiliko katika mawasiliano.
- Kufanya utafiti kuhusu vitu vya mawasiliano vilivyokusanywa na matumizi yake
- Kufafanua na kujenga uelewa kuhusu matumuzi sahihi ya teknolojia za mawasiliano.
- Kuonyesha vitu vya mawasiliano vilivyokusanywa.
- Kulinda na kuhakikisha usalama wa vitu vya mawasiliano vilivyokusanywa.
- Kueneza na kuendelea vitu vya mawasiliano vilivyokusanywa
- Kuchapisha makala kuhusu vitu vya mawasiliano vilivyokusanywa.
Aina ya vitu vilivyokusanywa
- Vitu vya kale vya mawasiliano.
- Vitu vya mawasiliano ya posta.
- Vitu vya mawasiliano ya simu.
- Vitu vya utangazji.
Saa za kazi
Makumbusho yako wazi kati ya Jumatatu na Ijumaa kuanzia saa 3 dakika thelathini (3:30) asubuhi hadi saa tisa (9) mchana
Kiinglilio ni
Bure
Namna ya kujitolea vitu kwa maonyesho
Vitu vilivyokusanywa kwenye Makumbusho ya Mawasiliano ni nyenzo muhimu zinazowezesha wanaotembelea kujifunza, kutafiti na kutambua uwepo wa mawasiliano na thamani yake kwa umma kupitia maonyesho. Wale wanaotake kujitolea vitu vya mawasiliano kwa ajili ya maonyesho wanaombwa kuwasiliana na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania kuhusu utaratibu. Kuna fomu maalum ya kujaza kwa wanaopenda kujitolea vitu vya mawasiliano.