VILABU VYA KIDIJITI
Vilabu vya kidijiti ni vikundi vya Wanafunzi vya uhamasishaji wa masuala ya Kidijiti vilivyoanzishwa katika taasisi za elimu kwa lengo la kushirikishana ujuzi wa masuala ya kidijiti kwa wanafunzi na kuunda majukwaa ya kujengeana uwezo.
Huundwa na wanafunzi wasiopungua wawili ambao ndio watakuwa viongozi na Mlezi mmoja ambaye ni mtumishi ambaye atakuwa mwakilishi na msimamizi wa viongozi na wajumbe wa klabu kwenye Taasisi inayohusika
Umuhimu
- Kukuza maarifa kuhusu mawasiliano kwa vijana (Raia wa kidijiti);
- Kuhimiza vijana kutimiza wajibu wao wanapotumia bidhaa na huduma za mawasiliano;
- Kueneza maarifa yaliyopatikana kwa wenzao na familia;
- Kuimarisha utamaduni wa kuzingatia usalama mtandaoni;
- Kuwahamasisha vijana kujiajiri kupitia mawasiliano.
Faida
- Kuongeza maarifa katika sekta ya mawasiliano;
- Kutambuliwa kwa wanachama na TCRA, mfano, kupewa vyeti.
Wajibu wa TCRA
- Kuhamasisha uanzishwaji wa Klabu za Kidijiti katika Vyuo Vikuu;
- Kuwaelimisha wanachama wa kikundi, masuala ya kidijiti;
- Kusambaza Elimu kwa Umma kuhusu mawasiliano;
- Kuandaa semina/mijadala/mashindano, katika kuwezesha vilabu kukutana na kujadili masuala ya mawasiliano;
Wajibu wa Vilabu vya Kidijiti
- Kuhamasisha wanafunzi katika Vyuo Vikuu kujiunga na klabu;
- Kujadili masuala mbalimbali ya mawasiliano;
- Kushiriki semina za Mawasiliano ili kuboresha ujuzi wa mawasiliano;
- Kuhudhuria/andaa midahalo ya mawasiliano ndani na nje ya shule;
- Kuwashirikisha maarifa ya mawasiliano wanafunzi wengine na jamii kwa ujumla.
Wajibu wa Chuo Kikuu
- Kuvitambua Vikundi vya Kidijiti vilivyoundwa
- Kutoa idhini kwa shughuli za vilabu vya Kidijiti kufanyika ndani/ nje ya eneo la Chuo Kikuu
Matokeo Yanayotarajiwa
- Ongezeko la Wakufunzi
- Kuwa na Mawanda ya kuelimishana juu ya masuala yanayohusika
- Kuanzishwa kwa Vilabu vya Kidijiti katika Taasisi za Elimu ya Juu
- Kuwa na mwendelezo wa upatikanaji Elimu
- TCRA kufahamika zaidi
- Kuwa na raia wa Kidijiti wenye kuwajibika; na ongezeko la vijana wenye kuipenda TEHAMA hatimaye kuboresha mtazamo wa watumiaji wa huduma na Bidhaa za mawasiliano.
TCRA inashirikiana kwa karibu na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia pamoja na taasisi nyingine ili kuunda vilabu vya kidijiti, lengo likiwa ni kuongeza uelewa kwa wanafunzi wanaosoma masomo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kuhusu fursa zilizopo kwenye mitandao duniani.
Kwa maelezo zaidi, tafadhali wasiliana nasi kupitia anwani ya baruapepe digitalclubs@tcra.go.tz