JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA

TAASISI YENYE VIWANGO VYA ISO 9001: 2015

Semina ya Uchumi wa Kidijitali Kwa Watunga Sera – Zanzibar

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mnamo mwezi Machi 2022 iliendesha mafunzo ya kujenga uelewa kwa viongozi wa Serikali kuhusu uchumi wa kidijitali. Semina hiyo ya siku nne iliwahusisha viongozi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, ikifanyika kuanzia tarehe 8 Machi, 2022 hadi tarehe 11 Machi, 2022 Zanzibar.

Katibu Mkuu Kiongozi wa Tanzania, Balozi Hussein Katanga (wa nne kutoka mstari wa kwanza kulia), akionekana katikati ya picha ya pamoja iliyopigwa hivi karibuni mjini Zanzibar wakati wa Semina ya Uchumi wa Kidijitali iliyohudhuriwa na Watunga Sera, Wafanya Maamuzi wa Tanzania wakiwemo Mawaziri na Makatibu wakuu. Dhumuni la Semina hiyo lilikuwa kuhimiza azma ya Tanzania ya kuwa Nchi iliyobadilika kidijitali katika sekta zote, ili kukabiliana na changamoto za maendeleo ya TEHAMA duniani. Mheshimiwa Nape Moses Nnauye (Mb), Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari (wa tatu kushoto mstari wa kwanza), Mhe. Innocent Bashungwa (Mb), Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa) (wa pili kutoka mstari wa kwanza kushoto), Naibu Waziri wa Kilimo – Mhe. Antony Peter Mavunde (Mb) (wa kwanza kulia mstari wa kwanza), Dk. Jim Yonazi Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari (wa tatu kulia mstari wa kwanza), na Dkt. Jabiri Bakari, Mkurugenzi Mkuu wa TCRA. (wa tatu kutoka safu ya pili kulia), walikuwa miongoni mwa washiriki wa Semina hiyo

Je, una Maswali yoyote juu ya Sekta ya Mawasiliano?
Tuma Mrejesho na Malalamiko!

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imejidhatiti kutoa huduma bora kwa wateja na wadau wake wote.

Tuma Mrejesho na Malalamiko!