Sheria Na. 12 ya mwaka 2003 iliyoianzisha TCRA inaipa Mamlaka wajibu katika majukumu yafuatayo:
- Kukuza ushindani bora na uchumi wenye tija;
- Kulinda maslahi ya watumiaji;
- Kulinda mitaji ya Watoa Huduma wenye ufanisi;
- Kukuza upatikanaji wa huduma zinazodhibitiwa kwa watumiaji wote wakiwamo wenye kipato kidogo, walioko vijijini na watumiaji walio na walioko katika mazingira magumu;
- Kuimarisha Elimu kwa Umma, uelewa na ufahamu wa huduma zinazosimamiwa na TCRA, ikiwa ni pamoja na:
(i) Haki na wajibu wa watumiaji na watoa huduma zinazosimamiwa;
(ii) Namna ya kuwasilisha malalamiko na migogoro na utaratibu wa utatuzi wake; na
(iii) Kazi na majukumu ya Mamlaka kwa kuzingatia umuhimu wa kulinda na kutunza mazingira.



