Banda la TCRA Kimbilio kwa Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano

Na mwandishi wetu, DAR ES SALAAM.
BANDA la Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) limekuwa kimbilio la watumiaji wa huduma za Mawasiliano, kwenye Maonesho ya 49 Kimataifa ya Biashara (Sabasaba) 2025, jijini Dar es Salaam.
TCRA ni moja ya taasisi zaidi ya 200 za Serikali zinazoshiriki katika maonesho hayo yanayoendelea pembezoni mwa barabara ya Kilwa Wilayani Temeke ambapo Maonesho ya Kimataifa ya Biashara yanaendelea. Banda la TCRA katika maonesho hayo limekuwa kivutio ambapo Fursa zilizopo kwenye Sekta ya Mawasiliano hufafanuliwa na Ufumbuzi wa changamoto zote za watumiaji wa huduma zamawasiliano hutolewa hapo (One stop Centre).
Pamoja na masuala mengine TCRA, inashiriki kutoa historia ya ukuwaji wa sekta ya Mawasiliamo nchini kupitia kifaa maalum cha Makumbusho ya Kidijiti ambapo sekta ndogo tatu za historia ya huduma za Kiposta na usafirishaji wa vifurushi na vipeto, huduma ya utangazaji wa redio na televisheni na huduma ya simu ya intaneti zimeelezewa kwa umahiri.
Watumiaji wa huduma za Mawasiliano ya simu na intaneti wenye changamoto mbali mbali, wanapata ufumbuzi wa matatizo yao moja kwa moja kwenye banda la TCRA ambapo, wanapata maelezo kutoka kwa Umoja wa Mafundi Simu Mkoa Dar es Salaam na Pwani (U.M.S.D.P) na Chama cha Wakalimani wa lugha ya alama Tanzania (Tanzania Sign Language Interpreter), Wasajili wa Vikoa vya Taifa (Dot TZ Domain Names) KILIHOST na ZESHA waliopo kwenye banda la TCRA. Pia Kampuni zinazotoa huduma ya simu za mkononi wote wapo katika maonesho hao, zikiwemo Kampuni ya Mawasiliano Tanzania (TTCL), Vodacom, Tigo na Halotel.
Wananchi kutoka sehemu mbalimbali za Nchi wanaomiminika kwenye banda la TCRA, pia wanafaidika na elimu ya matumizi bora na salama ya mitandao, ikiwemo mambo muhimu ya kuzingatia, ili kujilinda unapotumia huduma za mawasiliano ya simu na intaneti.
Katika kutoa elimu hiyo, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Mahusiano kwa TCRA, Ndugu Rolf Kibaja amehimiza wananchi kuchangamkia fursa za kiuchumi za biashara mbalimbali zilizopo mtandaoni pia amewasihi wanapopata ujumbe wakitapeli, kwa mfano, “Ile pesa tuma kwenye namba hii, Usipige Simu imeharibika spika”. Tuma Namba ya tapeli aliyekupigia au kukutumia Ujumbe wa Wizi kwenda 15040 BURE.
Ndugu Kijaba amesihi Wananchi kuwa makini wanaputumia huduma za mawasiliano ili kuepuka wizi, ulaghai na utapeli. Pia amewashauli Kuhakiki Idadi ya Laini za simu zilizo Sajiliwa kwa Kutumia Namba ya Kitambulisho cha Taifa Kutoka NIDA, kwa Kubofya, *106#, arafu, utaona namba 1 hadi 5, kwenye Ujumbe wa simu yako. Na. 1. Angalia Usajili 2. Namba zilizosajiliwa na NIDA yako. 3. Namba Zilizosajiliwa Mitandao Yote kwa NIDA yako, 4. Kufuta Usajili, 5. Kuhakiki au Kuongeza Namba.
Mtambo wa Utambuzi, Ufuatiliaji na Udhibiti Masafa pia upo kwenye banda la TCRA. Mhandisi wa Masafa TCRA Osward Joseph alielezea wananchi utendaji kazi wa Mtambo wa Utambuzi na Upimaji wa Masafa, (Mobile Frequency Spectrum Monitoring Station), pamoja na Kifaa ha Upimaji wa Mionzi ya Mawasiliano (Electric and Magnetic Field Radiation Metre), ambapo kilionesha mionzi ikiwa chini kabisa ya viwango, kwahiyo salama kwa Wananchi na watumiaji wa huduma.
Sekta ya Mawasiliano imezidi ku paa kwa ufanisi ambapo Zaidi ya laini za simu milioni Tisini na Laki Nne (90.4 m), zimesajiliwa nchini kote hadi Machi, 2025 ambapo mawasiliano ya meshawafikia zaidi ya asili mia 93.3 ya wananchi. Taarifa ilitotolewa hivi karibuni na Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Dkt. Jabiri Bakari imebainisha Zaidi ya milioni Sitini na Sita nukta Tano (66.5 milioni) wananufaika na huduma ya kutuma na kupokea pesa, na wengine 49.3 milioni wapo kwenye huduma za mtandao wa inteneti.
Utafiti uliofanywa na Shirika la Mawasiliano Duniani (International Telecommunication Union (ITU- Global Index) Jijini Geneva Uswizi karibuni umebainisha kwamba Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, imewekwa katika ngazi ya kwanza (Tier I) ambayo niya juu kabisa duniani katika usalama mtandaoponi. Pia Tanzania ni moja wapo ya Nchi 46 Duniani zinazoiongoza kwa kuzingatia Kanuni ya Usalama Mtandaoni .ni wa Kwanza kwa Ubora kwa Nchi ya Afrika Mashariki na Kati na a Pili kwa Usalama kwenye Mifumo ya Mtandao . Kipindi hiki kimeshuhudia kuanzaishwa kwa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi kuhakikisha taarifa binafsi ya watumiaji wa huduma za mawasiliano zinalindwa.
Maonesho hayo ya 49, ya Kimataifa ya Biashara Sabasaba ya Dar es salaam yenye kauli mbiu “ Sabasababa 2025 Kijigitali Zaidi” yanazinduliwa rasmi leo hii, Tarehe 7/7/2025 pembezoni mwa Barabara ya Kilwa, Wilayani Temeke jijini - Dar es Salaam.
Pamoja na takribani taasisi 200 za Serikali, kuna idadi kubwa ya kampuni na watu binafsi, Mikoa 12, Manispaa Zaidi ya 45, Wizara takribani 20, na Nchi mbalimbali zipatazo 23 kutoka nje ya Nchi.