JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA

TAASISI YENYE VIWANGO VYA ISO 9001: 2015

MKUTANO WA PILI WA BODI YA UBUNIFU WA KIDIGITALI WA ITU NA KONGAMANO LA UBUNIFU (28-30 OKTOBA, 2024)


MKUTANO WA PILI WA BODI YA UBUNIFU WA KIDIGITALI WA ITU NA K...

Ushirikiano wa Ubunifu na Ujasirimali (Innovation and Enterprenuarship Alliance for Digital Development) ulioanzishwa na Shirika la Mawasiliano Duniani (ITU) Januari mwaka 2023 kwa ajili ya kuweka mfumo wa kujenga uwezo, kuchochea na kupunguza pengo la ubunifu wa kidijitali (Digital Innovation Gap) kwa nchi wanachama. Uanzishwaji wa Ushirikiano huu ni sehemu ya maazimio ya Mkutano wa mwisho wa Maendeleo ya Mawasiliano Duniani (WTDC 22) uliofanyika Juni,2022 nchini Kigali, Rwanda.

Utendaji kazi wa Ushirikiano huu unahusisha:

  1. Bodi ya Wadau wa Usimamizi wa Bunifu (ITU Innovation Board) linaloongozwa na Mwenyekiti Dkt. Cosmas Zavazava, Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Mawasiliano ya ITU na wajumbe 23 ambapo Dkt. Jabiri Kuwe Bakari, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ni mjumbe wa Bodi hii.
  2.  Mtandao wa vituo vya ubunifu (ITU Acceleration Centres) ambavyo vimegawanywa kwenye ngazi ya Kidunia, Kikanda na Kitaifa (global, regional and national acceleration centres) ambapo Tanzania imepewa nafasi ya kuanzisha Kituo cha Kitaifa kinachosimamiwa na Tume ya TEHAMA;
  3. Maabara ya Mapinduzi ya kidijitali iliyoanzishwa Geneva, mwezi Mei,2023 kwa ajili ya kutoa msaada wa kifundi kwa vituo vya ubunifu.

Mkutano wa pili wa Bodi umefanyika kwa siku moja Valletta, Malta tarehe 28-10-2024 sambamba na Kongamano la Ubunifu kuanzia 28-30 Octoba, 2024 na umehudhuriwa na mjumbe wa Bodi, Dkt. Jabiri Kuwe Bakari, Mhandisi Mwesigwa Felician, Mkurugenzi wa Masuala ya Kisekta pamoja na Mr. Ezra Mmakasa kutoka TCRA. Aidha kutoka taasisi zingine ni pamoja na  Dkt. Nkundwe Mwasaga, Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya TEHAMA pamoja na Dkt. Florence Rashid kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma.

Lengo la Mkutano huu  wa Bodi ilikuwa ni kupata na kujadili ripoti ya utekelezaji kwa kipindi cha miezi sita katika kutekeleza programu hii.  Kwa kuwa Tanzania inaanzisha kituo cha ubunifu kwa uratibu na ushirikiano kutoka ITU, itapata fursa ya kuendesha kituo kwa utalaam na kimkakati ili kuchochea mabadiliko ya ikolojia nzima ya bunifu ndani ya nchi, kikanda na duniani kwa ujumla.

Bodi imejadiliana mambo kadhaa ikiwa ni pamoja na :

  • Njia za kukuza bunifu mbalimbali za TEHAMA ikiwa ni pamoja na kuangalia upatikanaji wa rasilimali fedha na watu. 
  • Kukuza ushirikiano kati ya vyuo vikuu vya ubinifu na taasisi zinazojihusisha na ubunifu.
  • Kuwa na mfumo utakaowezesha ubadilishanaji wa taarifa za vituo vya ubunifu duniani.
  • Umuhimu wa kulinda haki miliki za bunifu mbalimbali na kuzikuza ili wabunifu wapate faida za kazi zao.
  • Ushirikishwaji wa serikali katika kusimamia na kukuza vitu vya ubunifu wa TEHAMA.
  • Kuwa na vipaumbele kwenye ubunifu mfano bunifu zinazolenga kusaidia upatikaji wa huduma sehemu zisizo na huduma (unserved and underserved).

Kwa ujumla Mkutano huu umekuwa wa tija sana kwa kubadilishana mawazo na uzoefu wa kukuza ubunifu wa kidigiti katika nchi yetu.

Je, una Maswali yoyote juu ya Sekta ya Mawasiliano?
Tuma Mrejesho na Malalamiko!

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imejidhatiti kutoa huduma bora kwa wateja na wadau wake wote.

Tuma Mrejesho na Malalamiko!