JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA

TAASISI YENYE VIWANGO VYA ISO 9001: 2015

Ujenzi Makao Makuu ya PAPU, Arusha Wafikia hatua nzuri.

Na Mwandishi Wetu

Mandhari ya jiji la Arusha hivi karibuni itabadilika mara baada ya kukamilika kwa ujenzi wa jengo la kisasa linalojengwa kwa ubia kati ya Serikali ya Tanzania kupitia Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na Umoja wa Posta Afrika (PAPU).

Ujenzi wa jengo hilo lililobatizwa jina la “PAPU House” litakalokuwa na Ofisi za Makao Makuu ya Umoja wa Posta Afrika (PAPU); hadi sasa umefikia asilimia 80.

Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Dk Jabiri Bakari, akikagua ujenzi wa jengo hilo huku akiwa ameambatana na Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka hiyo na Mwenyekiti wake, Dk Jones Kilimbe, alibainisha kuwa ujenzi huo unaendelea kama ilivyopangwa ambapo Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TCRA Dk. Kilimbe alibainisha kuridhishwa na kasi ya maendeleo ya ujenzi wa jengo hilo.

Dk. Kilimbe aliipongeza timu ya Menejimenti ya TCRA kwa usimamizi Madhubuti wa ujenzi Pamoja na wahandisi kwa kazi nzuri, na kuwataka kufanya kila wawezalo ili kukamilisha mradi huo kama ilivyopangwa.

Baada ya kukamilika kwake, jengo hilo litakuwa na ofisi za wafanyakazi wa Menejimenti na Utawala wa PAPU wanaowakilisha nchi zote 45 wanachama wa Umoja huo, uliopo chini ya mwamvuli wa Umoja wa Afrika (AU).

Jengo hilo linamilikiwa kwa uwiano wa asilimia 60:40 kati ya PAPU na TCRA mtawalia--litakuwa jengo refu zaidi Arusha, ambapo mbali na kuwa Makao Makuu ya PAPU pia litakuwa na Ofisi za Kanda ya Kaskazini za Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Ofisi za biashara, vyumba vya mikutano, vituo vya mafunzo, maduka makubwa, huduma za benki, na zaidi.

Mradi huo hadi sasa umetoa fursa za ajira kwa wenyeji na unatarajiwa kuwapatia watalii na watu wengine huduma muhimu za kiuchumi na kijamii zinazoendana na wakati.  Ujenzi wa jengo hilo ulianza Januari 2020.

Ujenzi wa jengo hilo ni sehemu ya mkakati wa PAPU, kupata uhuru wa kifedha katika kutekeleza shughuli zake za kila siku, badala ya kutegemea uendeshaji wa ofisi kwa michango kutoka kwa wanachama wake pekee.

Umoja wa Posta wa Afrika (PAPU) ni taasisi maalumu ya Umoja wa Afrika ikiwa na dhima ya kuratibu shughuli zote zinazolenga kuendeleza huduma za posta katika bara la Afrika.

Je, una Maswali yoyote juu ya Sekta ya Mawasiliano?
Tuma Mrejesho na Malalamiko!

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imejidhatiti kutoa huduma bora kwa wateja na wadau wake wote.

Tuma Mrejesho na Malalamiko!