JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA

TAASISI YENYE VIWANGO VYA ISO 9001: 2015

TCRA: “Waandaji Maudhui Binafsi Fufueni Umoja Wenu Kuwezesha Maudhui Bora”


TCRA: “Waandaji Maudhui Binafsi Fufueni Umoja Wenu Kuwezesha...

Dar es Salaam, 16 Oktoba 2023

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetoa wito kwa waandaji binafsi wa maudhui nchini kufufua umoja wao ili iwe rahisi Serikali kuwasaidia katika kukuza uandaaji na upatikanaji wa maudhui bora nchini.

Akizungumza kwenye kikao-kazi na waandaji maudhui binafsi kwenye Ofisi za TCRA jijini Dar es salaam, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania Dkt Jabiri Bakari aliwataka waandaji binafsi wa maudhui kudumisha umoja wao kwani ndiyo nyenzo ya kuwawezesha kukua na kupata usaidizi unaowezekana.

Dkt. Jabiri aliwapongeza watayarishaji hao kwa kazi nzuri wanayofanya na kutoa rai ya uhuishwaji wa Chama cha Watayarishaji Maudhui wa Kujitegemea (TAIPA) ili irahisishe kazi ya uratibu na kuwezesha tasnia ipasavyo.

"TCRA inatambua umuhimu wa vyama hizi vya tasnia hasa katika kuwakilisha sauti ya wanatasnia, hivyo, ni muhimu mkafufua shughuli zenu na kuwa pamoja ili iwe rahisi kuongeza mahusiano kati ya taasisi na kuongeza urahisi wa uratibu wa shughuli zenu za uandaaji wa maudhui bora na kukuza tasnia. TCRA inatambua umuhimu wa tasnia ya maudhui ya ndani katika kuleta ajira na maendeleo. Kwa hiyo, tunaunga mkono juhudi za watayarishaji wa kujitegemea katika kukuza tasnia hii," alisema Dkt. Bakari.

Kikao hicho kilihudhuriwa na watayarishaji maudhui wa kujitegemea kutoka mikoa mbalimbali nchini Tanzania. Watayarishaji hao walijadili masuala mbalimbali yanayohusu tasnia ya maudhui ya ndani, ikiwa ni pamoja na changamoto zinazokabili tasnia hiyo na fursa zinazopatikana.

Je, una Maswali yoyote juu ya Sekta ya Mawasiliano?
Tuma Mrejesho na Malalamiko!

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imejidhatiti kutoa huduma bora kwa wateja na wadau wake wote.

Tuma Mrejesho na Malalamiko!