JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA

TAASISI YENYE VIWANGO VYA ISO 9001: 2015

BODI YA WAKURUGENZI UCC YAPEWA DARASA NA TCRA


BODI YA WAKURUGENZI UCC YAPEWA DARASA NA TCRA

Na Mwandishi wetu.

UJUMBE wa bodi ya wakurugenzi wa Tume ya Mawasiliano Uganda  (UCC) umefanya ziara ya siku moja ofisi za Mamlaka ya Mawasiliano TCRA, jijijni Dar Es Salaam  kwa ajili ya kujifunza namna TCRA inavyosimamia mfumo wa Leseni za Huduma za Mawasiliano nchini.

Ujumbe huo toka Uganda umeongozwa na Mwenyekiti wa Bodi hiyo Dkt. Charity Mulenga ambaye yeye na wajumbe wa Bodi hiyo wameteuliwa hivi karibuni kuongoza Tume ya Mawasiliano Uganda.

Akiukaribisha Ujumbe huo Mkurugenzi wa Huduma za Sheria TCRA Dkt. Philip Filikunjombe, aliwapongeza kwa kuteuliwa kwao kuongoza Tume hiyo; “Karibuni Mamlaka ya Mawasiliano na Tanzania, Pia hongereni kwa kuteuliwa kuongoza Tume ya Mawasiliano na nawatakia kila la kheri kwenye kutekeleza majukumu yenu..”

Dkt. Filikunjombe aliwapa historia fupi kuhusu TCRA na maboresho makubwa yaliyofanyika kwenye sekta hasa utaratibu wa maombi ya leseni kupitia mfumo wa Tanzanite Portal ambao kwa kiasi kikubwa umerahisisha utoaji wa leseni kwa watoa huduma za mawasiliano nchini. “Utaratibu wa utoaji wa Leseni kwasasa unafanyika kidijitali haimlazimu mteja kuja ofisi za TCRA, anaanzisa mchakato akiwa kwake na atapata leseni akiwa hapohapo kwake kupitia mfumo huu wa Tanzaniate Portal”

Nae Mhandisi Mwesiga Barongo Meneja wa Kitengo cha Utekelezaji na Ufuatiliaji akifanya uwasilishaji juu ya Mfumo wa Leseni kutaniko alielezea hatua mbalimbali TCRA ilizozichukua kuboresha utoaji wa Leseni na ubora wa huduma. “Kuanzia mwaka 2021 TCRA ilichukua hatua za makusudi kuboresha namna ya utoaji wa leseni kwa kunzisha mifumo ya kidijiti kama vile Tanzanite Portal”

“TCRA kwasasa inaendesha shuguli zake kidijitali kwakuwa mifumo yote ya ndani ni ya kidijiti” alisema Mhandisi Barongo. Kwa siku za karibuni TCRA imeendelea kuboresha utoaji wa huduma kwakuwa na mifumo mingi inayorahisha kazi na kuhudumia wateja kama vile dawati la huduma linawawezesha wateja kuhudumiwa bila kulazimika kufika ofisi za TCRA kwa saa 24.

Nae Mhandisi Iddi Mtanga Meneja wa Kitengo cha TEHAMA alisema Kwasasa kuna mfumo wa Usimamizi wa Mawasiliano ambao unatoa taarifa kwa muda kamili juu ya mifumo na huduma zitolewazo na watoa huduma.

“Hapo mwanzo mfumo wetu ulikuwa na uwezo wa kupata taarifa kwa watoa huduma wa simu pekee lakini kwasasa maboresho makubwa yamefanyika kuuwezesha mfumo kupata taarifa kwa watoa huduma wote kuanzia simu, utangazaji, posta na intaneti” aliongezea Mhandisi Mtanga.

Dkt. Mulenga akitoa shukrani kwa Menejimenti ya TCRA alisema “Imekuwa faraja kukubaliwa na kuweza kupata taarifa na maboresho mliyoyafikia katika kipindi kifupi. “Sisi kama Bodi mpya tumechukua mengi ambayo tutaenda kuyafanyia kazi na kuboresha huduma za mawasiliano Uganda” Dkt Mulenga.

Aliongeza kuwa Maabara ya kisasa ya kupima vifaa vyakielektroniki itakuwa msaada mkubwa kwa nchi za jirani ambazo hazijawekeza kama Tanzania.

Mamlaka ya Mawasiliano imekuwa ikipokea wageni kutoka nchi mbalimbali za ukanda wa Afrika mashariki na hata zile za SADC na Magharibi wanaokuja kujifunza namna TCRA inavyofanya maboresho ya kiutendaji. Kwasiku za hivi karibuni TCRA imeweza kupokea wageni toka nchi kama vile Kenya, Afrika ya Kusini, Visiwa vya Comoro, Uganda, Malawi na Mali.

Je, una Maswali yoyote juu ya Sekta ya Mawasiliano?
Tuma Mrejesho na Malalamiko!

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imejidhatiti kutoa huduma bora kwa wateja na wadau wake wote.

Tuma Mrejesho na Malalamiko!