Wataalamu wa Chuo Kikuu cha Midland Zimbabwe Wachota maarifa TCRA

Na Mwandishi Wetu.
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imeendelea kuwa taasisi muhimu ya mafunzo barani Afrika kutokana na kuwa kivutio kwa taasisi nyingine za mawasiliano, wadau wa mawasiliano na wanafunzi na kutoka vyuo vikuu mbalimbali.
Hilo linadhihirika baada kuendelea kupokea wageni kutoka nchi mbalimbali kwajili ya mafuzo na kubadilishana uzoefu katika usimamizi wa sekta ya mawasiliano.
TCRA imepokea wataalamu wa mawasiliano kutoka Chuo Kikuu cha Midland State cha nchini Zimbabwe, waliofika Ofisi ya Makao Makuu ya TCRA Januari 29, 2024 kwa ziara ya mafunzo ya siku tatu ikilenga kubadilishana uzoefu kuhusu usimamizi wa sekta ya mawasiliano.
Wakizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Mamalaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt Jabiri Bakari baada ya kumaliza mafunzo hayo wataalamu hao wamesema walishauriwa na Mamlaka ya Posta na Simu nchini Zimbabwe (POTRAZ) kuja TCRA kupata kile walichokihitaji.
Ujumbe huo ulioongozwa na Prof Laurine Chikoko Mkurugenzi Mtendaji wa Utafiti na uvumbuzi Midlands State University, ulitoa shukrani kwa TCRA kwa ushirikiano na uzoefu waliopata, ambao wamesema utaenda kuimarisha utendaji wao.
Katika siku tatu za uwepo wa wataalamu hao hapa nchini wamejifunza kuhusu simu na intaneti, huduma za posta na usafirishaji vifurushi na vipeto,na ukusanyaji na upangaji taarifa.